Taarifa ya Mwenyekiti

Wapendwa Washikadau,

Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, nina furaha kubwa ya kuwawasilishia utendakazi wa kifedha wa Shirika la mwaka uliomalizikia tarehe 31 Desemba, 2020.

Mwaka wa 2020 ambao hautasahaulika, usio kifani na usioweza kulinganishwa. Ulimwengu uliathiriwa na tandavu ambalo kizazi cha sasa hakijawahi kupitia. Tandavu hili limepindua dunia juu chini, na kulazimisha mataifa kadhaa kufunga baadhi ya shughuli au kufunga shughuli zote kabisa. Usafiri wa ndege, za humu nchini na zile za kimataifa, ama ulisimamishwa au ulifanywa kuwa vigumu zaidi, na baadhi ya viwanda vilifungwa huku vingine huenda vikaanguka.

Hatua hizi zimevuruga maisha yetu kwa njia ambayo yeyote miongoni mwetu hajawahi kupitia awali, kuzuia biashara na mifumo ya usambazaji wa bidhaa, na kusababisha watu wengi kupoteza kazi au kupunguziwa mishahara, kufanya kazi nyumbani, au kuenda likizo bila malipo, huku biashara zikijaribu kumudu janga hili la kipekee. Hata hivyo, kuvurugwa kwa shughuli kulikuwa na matokeo mengine chanya; hali hii ililazimisha biashara kuweka mikakati mipya kwa kuongeza kasi ya mageuzi ya kidijitali.

Download Full Chairmain's Statement